Habari za Michezo Ulaya 04.08.2024
MICHEZO
Published on 04/08/2024

Atletico Madrid wapo kwenye mazungumzo na Manchester City kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wao wa Argentina Julian Alvarez, 24. (Athletic - usajili unahitajika)

Arsenal pia wanafikiria kumnunua Alvarez, lakini The Gunners huenda wakalazimika kuwauza wachezaji zaidi ili kufadhili ununuzi wake. (Mirror)

Newcastle wanatumai kufanikisha mpango wa kumnunua beki wa Uingereza na Crystal Palace Marc Guehi, 24. (Mail)

Palace wameiambia Newcastle kwamba wanataka kulipwa £50m pamoja na nyongeza ili kumuuza Guehi. (Football Insider)

Bournemouth wanasisitiza kwamba Tottenham italazimika kutimiza masharti yao ya pauni milioni 65 ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Solanke, 26, msimu huu. (Mirror)

The Cherries wanamtaka mshambuliaji wa Aston Villa na England chini ya umri wa miaka 21 Cameron Archer, 22, kama mbadala wa Solanke. (Tem talk)

RB Leipzig wameidokezea Barcelona kwamba watahitaji kuboresha masharti kuhusu ombi lao la euro 61m kumnunua kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 26, ili kukamilisha dili. (90 min)

 

Comments
Comment sent successfully!