HABARI ZA MICHEZO ULAYA 04.10.2024
MICHEZO
Published on 04/10/2024

Paris St-Germain wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah na watajaribu kumjaribu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye mkataba wake wa Liverpool unamalizika mwishoni mwa msimu huu, kwa mkataba wa miaka mitatu. (sun).

Liverpool wamemtambua fowadi wa Borussia Dortmund Karim Adeyemi kama mrithi wa Salah, na wako tayari kutoa dau la pauni milioni 41 kumnunua Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 22. (Bild - Deutsch)

Manchester United inaandaa ofa ya takriban pauni milioni 34 kumnunua winga wa Benfica mwenye umri wa miaka 25 na Uturuki Kerem Akturkoglu. (Fichajes – In Spanish)

Newcastle United wanataka kurejelea harakati zao za kutaka kumnunua beki wa kati wa England Marc Guehi mwezi Januari, huku wakitarajiwa kuwa Crystal Palace watakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

 

Chelsea inamtaka fowadi wa Colombia Jhon Duran, lakini Aston Villa wanataka zaidi ya £80m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (TeamTalks)

Barcelona na Juventus wanafuatilia hali ya winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, huku Manchester United ikiaminika kumthamini mchezaji huyo kwa pauni milioni 50. (Sun)

Mkufunzi wa Fenerbahce Jose Mourinho anagombea kuchukua nafasi ya Sean Dyche kama meneja wa Everton mara tu Dan Friedkin atakapomaliza kuinoa klabu hiyo. (Football Insider),.

Atletico Madrid wamemtambua mlinzi wa Chelsea na England Ben Chilwell, 27, kama lengo lao la hivi punde la uhamisho. (TeamTalks).

 

Newcastle United ni miongoni mwa walio mstari wa mbele kumsajili mshambuliaji wa Canada Jonathan David mwenye umri wa miaka 24 kutoka Lille. (GiveMeSport)

Mshambulizi wa Norway Erling Haaland, 24, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na Manchester City lakini anataka kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 100 kiongezwe. (TeamTalks)

Barcelona wanafanya usajili wa Haaland katika dirisha la uhamisho la 2025 kuwa kipaumbele chao. (SPORT - Spanish).

Sir Jim Ratcliffe atahudhuria mechi ya Ligi Kuu ya Manchester United huko Aston Villa Jumapili huku uvumi kuhusu mustakabali wa meneja Erik ten Hag ukiongezeka. (Mirror)

 

Comments
Comment sent successfully!