Manchester United wanajiandaa kumnunua Randal Kolo Muani, Real Madrid wanamlenga William Saliba wa Arsenal, huku Chelsea wakimtaka Victor Osimhen.
Manchester United wameandaa ofa ya pauni milioni 58.6 kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 25 Randal Kolo Muani. (Fichajes, via Teamtalk)
Real Madrid wanataka kumsajili beki wa Arsenal na Ufaransa William Saliba mnamo 2025, huku Los Blancos wakiwa tayari wanawasiliana na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Le 10 Sport - kwa Kifaransa)
Galatasaray watajaribu kuufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen kutoka Napoli kuwa wa kudumu, huku Chelsea wakiendelea kumsaka. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 atagharimu pauni milioni 68 mwezi Januari au pauni milioni 63 msimu ujao. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)