Dortmund Wasema iwe isiwe lazima Pascal Gross Wamutoe Brighton
MICHEZO
Published on 31/07/2024

Borussia Dortmund wanakaribia kumnunua Pascal Gross wa Brighton, Romelu Lukaku wa Chelsea akubali kukatwa mshahara ili kuhamia Napoli, The Blues na Aston Villa wamewasilisha ofa kwa Maximilian Beier.

Chelsea wanajadili mpango wa mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 31, kujiunga na Napoli, huku mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 25, akitarajiwa kuhamia klabu hiyo kwa mkopo. (Athletic - usajili unahitajika)

Lukaku tayari amekubali kukatwa mshahara na kusaini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo ya Serie A. (Ben Jacobs)

Brighton wamekubali mkataba wa £5.9m kumruhusu kiungo wa kati wa Ujerumani Pascal Gross, 33, kujiunga na Borussia Dortmund. (Guardian)

Comments
Comment sent successfully!