Viongozi wapya wa Syria lazima watimize ahadi za kuheshimu haki – Mjumbe wa UN
SIASA
Published on 19/12/2024

Ni muhimu uongozi mpya wa Syria utimize ahadi zake za kuheshimu haki za watu wa dini na makabila mbalimbali nchini humo, hayo yamesemwa na Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa, Geir Pedersen.

Pedersen, akizungumza na BBC mjini Damascus, amesema Wasyria wana "matumaini na hofu nyingi kwa wakati mmoja.”

Ametoa wito kwa pande zote, ndani na nje ya Syria, kufanya kila wawezalo ili kuleta utulivu nchini humo.

Utawala wa Bashar al-Assad ulipinduliwa chini ya wiki mbili zilizopita na muungano wa waasi unaoongozwa na Hayat Tahrir al-Sham, unaojulikana kama HTS, kundi la Kiislamu la Sunni ambalo linadai limeachana na itikadi kali za jihadi tangu lilipojitenga na al-Qaeda mwaka 2016.

HTS linatajwa kama shirika la kigaidi na UN, Marekani, EU, Uingereza na nchi nyingine.

Kiongozi wake ameachana na jina lake la wakati wa vita la Abu Mohammed al-Jolani na kurejea jina lake halisi la Ahmed al-Sharaa.

Waislamu wa madhehebu ya Sunni ni wengi nchini Syria, na Sharaa anasisitiza HTS ni vuguvugu la kizalendo la kidini lililo tayari kuvumilia vikundi vingine.

 

Comments
Comment sent successfully!