Polisi wa kutuliza ghasia katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo, walirusha gesi ya kutoa machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa wakiandamana kupinga madai ya udanganyifu katika uchaguzi siku chache baada ya washirika wawili wa upinzani kuuawa kwa kupigwa risasi.
Mamia ya watu, wakiwemo waandishi wa habari, walitawanyika huku polisi waliokuwa na silaha nzito wakiandamana kwenye barabara kuu siku ya Jumatatu. Shirika la habari la Reuters liliripoti baadhi ya maafisa wa polisi wakifyatua bunduki huku wakiwatawanya umati