MASHAMBULIZI YA ISRAEL
HABARI
Published on 22/10/2024

Baada ya wimbi la mashambulizi ya Israel kuzikumba benki zenye uhusiano na Hezbollah kote nchini Lebanon jana usiku, vyombo vya habari vya serikali ya Lebanon vimeripoti mashambulizi zaidi kusini mwa Lebanon katika saa chache zilizopita.

Wizara ya afya ya Lebanon imesema kuwa watu kadhaa wameuawa katika mashambulizi kote nchini humo na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) linasema kuwa linaendesha mashambulizi "kidogo, ya ndani, yaliyolenga" kusini mwa Lebanon.

Nchini Israeli, IDF inasema "takribani makombora 60" yamevuka hadi nchini kutoka Lebanon hadi sasa. Kwingineko, huko Gaza, IDF inasema "makumi ya wakazi" wameondoka kwenye kambi ya wakimbizi ya Jabalia, kaskazini, kupitia njia zilizopangwa.

Kama tulivyoripoti hapo awali, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuwa watu saba wameuawa kwenye kambi hiyo kufuatia operesheni ya Israeli.

Wakati huo huo, Marekani imeongeza juhudi za kidiplomasia kufufua mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza na Lebanon, ambapo mjumbe wa Mashariki ya Kati wa Marekani tayari yuko Beirut, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuelekea eneo hilo baadaye leo.

Afisa wa Hamas ameiambia BBC kwamba vuguvugu hilo huenda likaweka utambulisho wa kiongozi wake mpya, ambao unakusudia kumchagua Machi mwaka ujao,ukawa wa siri kwa sababu za kiusalama.

Comments
Comment sent successfully!