ICC imeahirisha kesi ya kuthibitisha mashtaka dhidi ya Joseph Kony
HABARI
Published on 12/09/2024

Kony amekuwa akitafutwa na mahakama ya ICC tangu mwaka 2005 kwa madai ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu (ICC) leo Alhamis imeahirisha kesi ya kuthibitisha mashtaka dhidi ya mbabe wa vita wa Uganda Joseph Kony, kutokana na kutokuwepo kwake, ikisema tarehe mpya itatangazwa baadaye.

Kony mwenye miaka 63, amekuwa akitafutwa na mahakama ya ICC yenye makao yake mjini The Hague tangu mwaka 2005, kwa madai ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya binadamu kufuatia utawala wa miongo mitatu wa vitisho uliofanywa na kundi lake la waasi la Lord's Resistance Army (LRA), katika mataifa kadhaa ya Afrika.

ICC ilitangaza miezi mitano iliyopita kuwa itafanya vikao mwezi Oktoba kuthibitisha makosa 36 dhidi ya Kony, ambaye hajulikani mahali alipo hivi sasa. Kikao cha awali cha mahakama kabla ya kesi, kiliamua kuahirisha kuanza kwa uthibitisho wa kusikilizwa mashtaka, hadi tarehe mpya ambayo itatangazwa baadaye, ilisema taarifa ya mahakama.

Usikilizaji uliahirishwa kufuatia Utetezi, Mashtaka na Ofisi ya Wakili wa Umma kwa ajili ya uchunguzi wa waathirika pamoja na mapendekezo ya tarehe ya uthibitisho wa kusikilizwa kwa mashtaka, ICC ilisema.

Comments
Comment sent successfully!