Wapinzani wa FARC watangaza kusitisha mapigano wakati wa COP16 Cali
HABARI
Published on 02/08/2024
 
Moja ya makundi makuu ya Wanajeshi wapinzani wa Mapinduzi ya Colombia (FARC) wametangaza kusitishamapigano wakati wa mkutano wa 16 juu ya bioanuwai (COP16) , uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba huko Cali, kusini magharibi mwa Colombia, katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.
"Ili kuhakikisha uendeshaji mzuri wa COP16, tunatoa amri ya kusimamishwa kwa operesheni za kijeshi dhidi ya vikosi vya umma katika jiji la Cali, kati ya Oktoba 11 na Novemba 6," limesema kundi hili pinzani dhidi ya FARC.
makao makuu (EMC), kundi kuu hasimu dhidi ya FARC ambalo halikukubali makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mnamo 2016 na waasi wa Marxist, lilitishia katikati ya mwezi wa Julai "kuzorotesha" mkutano wa kilele wa ulimwengu wa bioanuwai.
Waandalizi wanatarajia kuwasili kwa karibu wageni 12,000, waonyeshaji maonyesho na wanadiplomasia kutoka nchi 90, katika mji wa tatu wa Colombia, ambapo idadi kubwa ya vikosi vya usalama itatumwa.
EMC hivi karibuni imegawanyika kati ya wafuasi na wapinzani wa mazungumzo ya amani yaliyofanywa tangu mwisho wa mwaka 2023 na serikali ya mrengo wa kushoto ya Rais Petro.
Maeneo mawili jirani ya jiji la Cali, Cauca na Valle del Cauca (ambayo Cali ndio mji mkuu), ni ngome za "wapiganaji" wa EMC ambavyo vinakataa majadiliano haya.
Hali ya usalama katika maeneo hayo imezorota ghafla katika miezi ya hivi karibuni, na matukio ya usalama (hasa mashambulizi kadhaa) chini ya kilomita ishirini kutoka Cali, na makabiliano ya mara kwa mara na vikosi vya usalama.
Comments
Comment sent successfully!