WAZAZI WAANDAMANA TAHARUKI ONGEZEKO LA MATUKIO YA KUPOTEA WATOTO NA KUUWAWA MAENEO MBALI MBALI KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.
HABARI
Published on 23/07/2024
Ni takribani majuma kadhaa pamekuwa na Report za kupotea kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 9 kushuka chini hapa katika jiji la Dar es salaam, Jambo ambalo limekuwa likizua taharuki sana kwa wakazi wa jiji hilo. Na huku Selkali ikiendelea kufanya jitihada za kubaini chanzo cha tatizo hilo.
Mnamo Tarehe 23/07/2024. Hali imebadilika ghafla na kuwa taharuki kwa wakazi wa Kata ya Gongolamboto, Mtaa wa Ulongoni B.
Ambapo Wazazi wameandamana wakiomba shule zifungwe baada ya kupokea taarifa ya kupotea kwa mtoto mmoja na Kuuwawa kwa watoto wawili.
Hali hiyo imejitokeza leo majira ya Saa Sita na nusu Mchana, Kutokana na ongezeko la watoto kupotea katika jiji la Dar es salaam, hivyo wazazi hao waliandamana katika shule ya msingi ULONGONI B, iliyopo wilaya ya Ilala, kata ya Gongolamboto, hii ni baada ya kuripotiwa taarifa ya kupotea kwa mwanafunzi wa shule hiyo SHADRACK SALVATORY MEDADI alimaarufu GIFT, anayesoma darasa la nne shuleni hapo jana majira ya kumi na mbili (18h00)Jioni.
Katika maelezo yake baba wa mwanafunzi aliyepotea Bw. SALVATORY MEDADI CLEOTUS, Amesema kuwa mwanafunzi huyo Alitoweka tangu jana majira ya saa18:30 jioni, alipokuwa akirudi kutoka shuleni ambapo anasoma masomo ya ziada (Tuition) “hadi hivi sasa jitihada za kumtafuta hazijazaa matunda” , Alisema Salvatory.
Kulingana na hali hiyo ambayo imekuwa ikijitokeza kwa majuma kadhaa wazazi wameiomba serikali iingilie kati suala hilo, ili kuweka miundo mbinu rafiki kwa ajiri ya ulinzi wa watoto mashuleni ili kupunguza idadi ya upotevu na vifo kwa watoto.
Lakini baadhi ya wazazi wamewaomba wazazi wenzao wawajibike katika suala la kuwalinda watoto
pia wameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini Chanzo cha upotevu na mawaji kwa watoto wadogo, Na Hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wote watakao kutwa na hatia ya kushiriki katika Unyama huo. Imeripotiwa na Quine Tutu, RoyalQueen@utukufufm
Comments
Comment sent successfully!