Mjumbe wa Rais wa Marekani Joe Biden katika Mashariki ya Kati, Amos Hochstein amewasili Beirut katika jaribio la kutafuta mwafaka wa kumaliza vita kati ya Hezbollah na Israel.
Hii ni ziara ya kwanza ya Hochstein nchini Lebanon tangu Israel ilipoongeza kampeni yake ya kijeshi dhidi ya Hezbollah wiki nne zilizopita.
Katika safari zake za awali Hochstein amejaribu, na kushindwa, kuzuia vita ambavyo vimesababisha madhara makubwa kwa watu na miundombinu nchini Lebanon.
Alipofika Beirut, Hochstein alionya kuwa haikuwa kwa manufaa ya Lebanon kuwa na mustakabali wake unaohusishwa na migogoro ya kikanda, akimaanisha uhusiano wa karibu wa Hezbollah na Iran na uamuzi wake wa kuunga mkono Hamas katika mapambano yake na Israel.
Israel kwa muda mrefu imekuwa ikilalamika kwamba njia hii ilishindwa kuzuia Hezbollah kujenga uwepo wa kijeshi wa kutisha kusini mwa Lebanon na kurusha roketi kaskazini mwa Israeli, sababu inasema ilianza kampeni hii.
Lakini pande hizo mbili bado ziko mbali sana; haijabainika bado kama Israel au Hezbollah wako tayari kuacha mapigano.